Waasi wa Syria wamevamia mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria wa Aleppo, baada ya kulipua mabomu mawili ya kwenye gari wakipamba ba majeshi ya serikali siku ya Ijumaa, kulingana na mfuatiliaji wa vita vya Syria na wapiganaji.
Waasi walikuwa wakielekea katika mji wa Aleppo kwa siku kadhaa, wamekamata miji na vijiji kadhaa wakiwa njiani.
Syrian Observatory for Human Rights, ambayo inafuatilia vita, wamesema waasi wamelipua mabomu mawili ya kwenye gari katika ukingo wa magharibi wa mji huo siku ya Ijumaa.
Kamanda wa waasi ametoa ujumbe uliorekodiwa katika mitandao ya kijamii akiwataka wakazi wa mji huo kushirikiana na vikosi vinavyosonga mbele