Viongozi wa Marekani waomboleza kifo cha hayati Madeleine Albright

FILE - Hayati Madeleine Albright

Viongozi mbalimbali wanaomboleza kifo cha Madeleine Albright, mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, aliyefariki jumatano kutokana na Saratani. Alikuwa na miaka 84 kutokana na saratani.

Albright anakumbukwa kwa kushinkiza utawala wa aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton, kuchukua hatua dhidi ya rais wa Serbia Slobodan Milosevic, kuhusiana na uhalifu wa kivita uliotokea Balkans.

Kabla ya kuwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka 1996, Albright alikuwa balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa wakati wa utawala wa Bill Clinton.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema haya: "Waziri Albright alikuwa mtu wa kutoa mwelekeo kwa wengine. Alikuwa mkubwa wangu kama waziri wa mambo ya nje na huko Georgetown. Alikuwa mwenzangu na rafiki kwa miongo kadhaa. Ameacha kumbukumbu kubwa duniani na katika umoja wa mataifa. Nchi yetu na umoja wa mataifa wana nguvu kutokana na mchango wake. Alikuwa anatekeleza majukumu yake vipasavyo.

Akiwa waziri wa mambo ya nje, Albright alikuwa mwanamke wa wadhifa wa juu katika historia ya Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden ameamuru bendera kupepea nusu mlingoti hadi March 27.

Rais wa zamani Barack Obama, alimtuza Albright medali ya uhuru, ambayo ni ya juu zaidi kutolewa kwa raia, akisema kwamba maisha yake yalitoa motisha kwa wamarekani wote.