Kabla ya mkutano huo wa ECOWAS, Burkina Faso, Mali na Niger zimesisitiza tena kwamba hazitobadili uamuzi wao wa kujiondoa kwenye jumuiya hiyo, zikidai ECOWAS ni kibaraka wa Ufaransa.
Kuondoka kwa nchi hizo tatu kuna athari kubwa kwenye biashara huru na usafiri wa watu pamoja na ushirikiano wa usalama katika kanda hiyo ambapo makundi ya wanajihadi yanazidi kudhibiti maeneo katika kanda ya Sahel.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ni Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ambaye aliteuliwa kama mpatanishi na ECOWAS mwezi Julai.
Faye alisema wiki iliyopita kwamba alipiga hatua katika mazungumzo na nchi hizo tatu na kusema hakuna sababu kwa nchi hizo kutoshirikiana na nchi wanachama wengine, hasa kutokana na hali ya usalama.