Licha ya marufuku rasmi, Chadema kiliapa kusonga mbele na maandamano ya kupinga kile kinadai ni utekaji nyara na mauaji ya wanachama wake yanayofanywa na maafisa wa usalama.
Polisi wa kuzima ghasia walikuwa wamejipanga jijini kote wakiwa na mabomu ya kurusha maji ya kuwasha ili kuzuia mikusanyiko, na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu walikamatwa haraka pamoja na wengine kadhaa.
Baadaye Jumatatu jioni, chama hicho kiliandika kwenye mtandao wa X kwamba Mbowe na Lissu, pamoja na afisa mwingine mkuu wa chama, waliachiliwa kwa dhamana.
Hata hivyo, Mbowe “aliamua kubaki katika kituo cha polisi hadi wanachama na wafuasi wengine waliokamatwa wapewe dhamana,” Chadema kimesema.
Chama hicho kinaituhumu serikali ya Rais Samia Suluhu kuirejesha nchi kwenye mbinu za ukandamizaji za mtangulizi wake, hayati John Magufuli.