Mkataba wa amani wa mwaka 2005 uliyagawa mapato ya mafuta ya Sudan kati ya kaskazini na kusini, lakini mkataba wa kushirikiana utajiri unatarajiwa kufikia hatima yake baada ya kura ya maoni mwezi huu.
Wakusini watapiga kura January tisa iwapo wajitenge kutoka Sudan kaskazini, jambo ambalo litafuatiwa na uhuru wa eneo hilo.
Rosie Sharpe wa Global Witness anasema kuwa mkataba mpya utakapotengenezwa, utahitaji uwazi zaidi kuliko makubaliano yaliyopo hivi sasa, na kuongezea kuwa hakuna mwenye uhakika sudan inazalisha kiasi gani cha mafuta kwa wakati huu.
Na mkataba wowote mpya kati ya kaskazini na kusini ndiyo utakuwa ni mtihani wao, ambao huenda ukawa na madhara kwa nchi, suala hili linahitaji kushughulikiwa kikamilifu ili wasonge mbele.
Global Witness inaripoti kuwa takwimu kuhusu mafuta zilizochapiswaha na serikali ya Sudan ni tofauti na zile zilizotolewa na kampuni kubwa ya uchimbaji mafuta ya China National Petroleum Corporation.
Kiwango cha uzalishaji mafuta kilichoripotiwa na kampuni ya China ni kati ya asilimia tisa na 25 juu ya kile ambacho kimeripotiwa na serikali huko kaskazini.