Waandaji wa kura ya maoni ya Sudan Kusini wanasema wako tayari kwa asilimia 100 kwa kura hiyo kufanyika jumapili hii.
Afisa wa juu wa tume ya kura ya maoni Chan Reec alisema jana jumatatu kuwa karibu watu millioni 4 wamejiandikisha kupiga kura. Reec amesema wapiga kura wengi ni watu wa Sudan Kusini huku asilimia ndogo kati yao wakiishi Sudan kaskazini au ulaya.
Amesema ugawaji wa masanduku ya kura karibu unakamilika na upigaji kura utaendelea licha ya kutokuwepo kwa fedha zilizoahidiwa na serikali kuu ya Sudan.
Wakati huo huo mchambuzi wa kisiasa Mobale Matinyi aliyezungumza na Sauti ya Amerika amesema hakutakuwa na uwezekano wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kulipuka kwasababu Kusini na kaskazini zinategemeana katika usafirishaji wa mafuta hayo.