Katika eneo la utambuzi, watafiti katika chuo kikuu cha Johns Hopkins kwenye kitengo cha Kimmel Cancer kilichopo Baltimore, Maryland wamefanya utafiti wa upimaji damu ambao unasaidia kutambua aina nane tofauti za saratani.
Saratani ni ugonjwa wa pili wa juu unaosababisha kifo duniani kote, na watu wengi hawatambui kuwa wana maradhi hayo mpaka pale dalili zinapojitokeza. Hili linaweza kubadilika kwa kupima damu ambayo hujulikana kama CancerSEEK.
Profesa katika chuo cha John Hopkins ambaye anashughulikia saratani na patholojia, Nickolas Papadopoulos anasema. “upimaji umeanzishwa ili watu wasisubiri mpaka waone dalili.
Hatimaye, hayo ndiyo matumizi ambayo tungependa kwa upimaji huu. Lakini tofauti nyingine ni: moja, ni upimaji mchanganyiko. Kugundua vyote DNA nap rotini, na hilo ni jambo la kipekee katika upimaji damu kwamba wanagundua aina mbali mbali ya uvimbe.”
Dr. Nickolas Papadopoulos anasema upimaji unaweza kugundua aina nane ya saratani zinazojulikana sana, na pia ni upimaji wa kipekee katika uwezo wa kutambua sehemu ambayo saratani ipo.
Yeye na timu yake katika kitengo cha Kimmel Cancer huko chuo kikuu cha Johns Hopkins waliangalia DNA na protini zinazohusishwa na saratani katika damu ya zaidi ya wagonjwa 1,000 wa saratani.
Upimaji damu ulionyesha kuwepo saratani kwa asilimia 70 ya kesi, na asilimia 7 tu ilikuwa ni majibu ambayo hayakuwa sahihi kutoka katika kundi la watu 812 ambao walikuwa na afya nzuri.
Kiwango kikubwa cha majaribio kinahitaji kufanywa, lakini Papadopoulos anasema kazi yao huenda ikaokoa maisha na fedha.
“Ni gharama kubwa kuwatibu watu katika hatua za mwisho za saratani. Madawa ni ghali sana.
Tunaamini kwamba kufanya upimaji wa mapema tunaweza kugundua saratani kwa watu ambao bado wana afya njema, hawana dalili na pengine saratani itakuwa katika hatua za awali kabisa, hivyo itakuwa rahisi kuwatibu na matibabu yake pia ni rahisi na tunaweza kuokoa maisha ukilinganisha na kuongeza tu muda wao wa kuishi,” amesema Papadopoulos.
Watafiri wana matumaini kuwa CancerSEEK hatimaye itakuwa sehemu ya utaribu wa kawaida katika uchunguzi wa kiafya kama njia mojawapo ya kugundua saratani katika hatua za awali kabisa.