Shirika la Habari la Uingereza (BBC), limeripoti Jumapili kuwa wanajeshi hao waliuwawa, baada ya kifaru chao kushambuliwa katika eneo la Afrin.
Waziri Mkuu Binali Yildirim, amesema kuwa wanamgambo hao walioshiriki katika shambulizi hilo "watalipa thamani ya uovu wao maradufu".
Mara moja baada ya waziri kutoa tamko hilo, ndege za kijeshi ziliangusha mabomu katika ngome za Wakurdi Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.
Operesheni ya Uturuki iitwayo "Olive Branch" ilizinduliwa Januari 20, ili kuwaondoa wanamgambo wa kikurdi wa YPG kutoka maeneo ya Afrin.
Kwa mujibu wa idara ya jeshi la Uturuki, wapiganaji wa YPG walishambulia kwa makombora kifaru kimoja cha jeshi lake katika eneo la Sheikh Haruz, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.