Tom Fletcher alizungumza na wakimbizi wakati wa ziara ya siku tisa nchini Sudan na Chad, akiapa kupaza sauti zaidi kwa kuwatetea na kuutaka ulimwengu kutoa msaada mkubwa zaidi.
“Sisi hatuonekani,” alisema, akiwasilisha ujumbe kutoka kwa walioathirika.
Sudan imetumbukia katika vita tangu Aprili 2023, vinavyolihusisha jeshi la serikali linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces( RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo.
Machafuko yameua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni 11, na kusababisha kile Umoja wa Mataifa umekielezea kama mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu katika historia ya hivi karibuni.