UN imesema katika taarifa yake kuwa mashambulizi dhidi ya UN na vikosi vya Afrika ya Kati yalitokea huko Dekoa, katika mkoa wa Kemo, na Bakouma, katika mkoa wa Mbomou, lakini haikutoa maelezo zaidi.
Msemaji wa Katibu Mkuu Antonio Guterres, Stephane Dujarric amesema mashambulizi dhidi ya walinda amani wa UN “yanaweza kuchukuliwa ni uhalifu wa kivita.”
Guterres, kwa mujibu wa taarifa, amezitaka mamlaka za Afrika ya Kati kuchunguza mashambulizi haya ya ‘kinyama’ na “haraka kuwachukulia hatua za kisheria wanaoendeleza mashambulizi hayo.”
Guterres amethibitisha tena nia ya dhati ya UN kufanya kazi kwa karibu na washirika wa kitaifa, kieneo na kimataifa, taarifa hiyo imesema, kwa ajili ya amani na utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Muungano wa Wazalendo Wanamageuzi, kikundi cha waasi ambacho kimekuwa kikipambana na serikali, Ijumaa kilifuta siku tatu za sitisho la mapigano, na kusema wataanza tena kusonga mbele na mpango wa kuingia mji mkuu, Bangui.
Wakati huo huo Faustin Archange Touaderarais wa nchi hiyo, amemshutumu kiongozi aliyemtangulia Francois Bozize, kwa kupanga mapinduzi.
Bozize, aliyewekewa vikwazo na UN na kupigwa marufuku kuwania urais, amekanusha tuhuma hizo.