Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:27

Upinzani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walalamika


Wanawake waandamana nje ya mji wa Bangui kwenye picha ya awali.
Wanawake waandamana nje ya mji wa Bangui kwenye picha ya awali.

Muungano wa upinzani kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati Jumapili umeomba uchaguzi uliopangwa kufanyika Decemba 27 usitishwe kutokana na ghasia kutoka kwa makundi ya wapiganaji zinazoendelea nje ya mji mkuu wa Bangui, lakini serikali imesema kuwa ni lazima zoezi hilo liendelee kama ilivyopangwa.

Jumamosi iliopita serikali ililaumu aliekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize kwa kupanga kupindua serikali baada ya kunyimwa nafasi ya kuwania kiti cha urais. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mapigano yamekuwa yakiendelea kwenye miji kadhaa uliwemo ule wa Mbaiki ulioko takriban kilomita 100 kutoka Bangui.

Muungano wa upinzani unaojulikana kama Cod2020, na ambao Bozize ni mwanachama unadai kuwa ghasia zimezuia wagombea wa urais na ubunge kufanya kampeni zao. Wanasema kuwa vifaa muhimu vya kampeni pia vimeharibiwa kwenye ghasia hizo wakati pia kukiwa na madai ya kutishiwa maisha.

Kupitia taarifa ya pamoja wamesema kuwa zoezi la uchaguzi haliwezi kufanyika kamwe kwa mazingira yaliopo nchini.

Mtayarishi: Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG