Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Waasi wasitisha mapigano ili kuruhusu uchaguzi mkuu kufanyika Jamhuri ya Afrika ya kati


Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera

Muungano wa waasi ambao wamekuwa wakipigana kwa lengo la kupindua serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati, umesema kwamba utasitisha vita kwa mda wa siku 3 ili kuruhusu uchaguzi mkuu nchini humo kufanyika.

Taarifa ya muungano huo wa waasi unaojiita wazalendo wa mabadiliko – CPC, ulioanza mapigano dhidi ya serikali ijumaa iliyopita, umetangaza kusitisha vita kote nchini kwa mda wa saa 72.

Uchaguzi wa Jamhuri ya Afrika ya kati umetajwa kuwa mtihani muhimu kwa nchi hiyo yenye matatizo makubwa ya usalama.

Muungano wa CPC uliundwa mwezi Desemba tarehe 19 na makundi yenye silaha, yanayomshutumu rais Faustin Archange Touadera, kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho kutwa, desemba 27 ili asalie madarakani.

Rais Faustin, anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.

Makundi ya wapiganaji yanadhibithi Theluthi tatu ya Jamhuri ya Afrika ya kati, ambayo sehemu kubwa ya watu ni maskini sana.

Serikali imemshutumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Francois Bozize kwa kupanga kupindua itawala wa Faustin Archange Touadera. Bozize amekana madai hayo.

Wapiganaji walijaribu kuingia mji mkuu wa Bangii, lakini wakazuiwa na wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa, MINUSCA.

Wapiganaji walijaribu kudhibithi mji wa nne kwa ukubwa wa Bambari, Jumanne, ulio kilomita 380, kutoka Bangii, lakini wakazidiwa nguvu na wanajeshi wa serikali kwa msaada wa walinda usalama wa umoja wa mataifa.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG