Kuongezeka kwa umri wa kuishi mwaka 2022 hasa kulitokana na kuondoka kwa janga la COVID, watafiti wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maambukizi ya Maradhi walisema Jumatano.
Lakini pamoja na ongezeko kubwa, umri wa kuishi Marekani umerejea tu katika kiwango cha miaka 77, miezi sita – hali iliyokuwepo miongo miwili iliyopita.
Umri wa kuishi ni makadirio ya wastani wa idadi ya miaka ya mtoto kuzaliwa katika mwaka fulani akitarajiwa kuishi, ikichukuliwa kuwa matukio ya vifo kwa muda huo yatabakia kama yalivyo
Muhtasari wa Takwimu zilizochukuliwa zinakadiriwa kuwa moja ya vipimo muhimu vya afya ya wananchi wa Marekani.
Mahesabu ya 2022 yaliyotolewa Jumatano ni ya awali, na yanaweza kubadilika kidogo wakati mahesabu hayo yakikamilishwa.
Kwa miongo kadhaa, umri wa kuishi uliongezeka kidogo karibuni kila mwaka. Lakini muongo mmoja uliopita, mwelekeo huo ulibakia ulivyo na hata kushuka katika baadhi ya miaka – hali iliyoelezewa kwa kiwango kikubwa kusababishwa na vifo vya matumizi mabaya ya dawa na kujiua.
Baadaye vikaja virusi vya corona, ambavyo vimewauwa zaidi ya watu milioni 1.1 nchini Marekani kuanzia mapema 2020. Kipimo hicho cha maisha marefu ya Wamarekani kiliporomoka, kikishuka kutoka miaka 78, miezi 10 mnamo mwaka 2019 kufikia miaka 77 mwaka 2020, na baadaye kufikia miaka 76, miezi 5 mwaka 2021.
“Kimsingi tumepoteza miaka 20 tuliyopiga hatua mbele,” alisema Elizabeth Arias wa CDC.
Kushuka kwa vifo vya COVID-19 kulipelekea mabadiliko ya kuongezeka kwa umri wa kuishi mwaka 2022.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP