Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:30

Biden apimwa na kukutwa na virusi vya Covid-19


Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia)
Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia)

Rais wa Marekani Joe Biden amepimwa na kupatikana  na virusi vya Covid-19. Kwa mujibu wa msemaji wa White House Karine Jean-Pierre, rais huyo ana dalili zisizo kali za ugonjwa huo.

Rais wa Marekani Joe Biden amepimwa na kupatikana na virusi vya Covid-19. Kwa mujibu wa msemaji wa White House Karine Jean-Pierre, rais huyo ana dalili zisizo kali za ugonjwa huo.

Jean Pierre amesema kwamba Biden ameanza kutumia dawa aina ya Paxlovid. Amesema kwamba rais huyo atazingatia kanuni za kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC, na atajitenga katika Ikulu, na kwendelea kutekeleza majukumu yake yote kutoka mle.

Mratibu wa masuala ya Covid wa ikulu ya Marekani, Dk Ashish Jha, amewaambia waandishi wa habari kwamba Biden, mwenye umri wa miaka 79, hakuwa na homa leo asubuhi, lakini akaongeza kwamba ana mafua, kikohozi kikavu na anahisi uchovu.

Mke wa rais Jill Biden amesema kwamba alipimwa leo Alhamisi na kupatikana bila virusi hivyo. Rais Biden amepokea chanjo kikamilifu, kama ilivyopendekezwa na CDC.

((BRIEF SLUG: BIDEN CRIME

Rais wa Marekani Joe Biden leo anatarajiwa kuzungumza kuhusu pendekezo la dola bilioni 37 la kupambana na kuzuia uhalifu nchini Marekani. White House ilitoa maelezo ya mpango huo hapo jana, kabla ya hotuba ya Rais Biden, ambayo ataitoa katika jimbo la Pennsylvania. Mpango huo unajumuisha karibu dola bilioni 13 kusaidia katika kuajiri na kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wapatao 100,000 katika miaka mitano ijayo. Iwapo bunge litaridhia, dola zingine bilioni 3 zitatumika kushughulikia mlundikano wa kesi mahakamani, kutatua kesi za mauaji na kuunda vikosi-kazi vya ndani ili kupunguza viwango vya mashambulizi ya bunduki. White House ilisema pendekezo la Biden litaongeza adhabu kwa usafirishaji wa dawa aina ya fentanyl na kuliuliza bunge kutunga sheria inayofanya masoko ya mitandaoni kuwajibika ikiwa yatauza bidhaa zilizoibwa. Mpango huo pia unajumuisha dola bilioni 15 kwa miji na majimbo, katika juhudi za kuzuia uhalifu wa kutumia nguvu na kutambua hali ambazo mashirika ya afya ya umma yanapaswa kukabiliana na hali zisizo za vurugu badala ya polisi. Sehemu nyingine ya mpango huo inazingatia huduma za afya ya akili na matumizi mabaya ya dawa za kulevya, pamoja na kuwapa watu wengi fursa ya kupata mafunzo ya kazi, elimu na makazi.

((BRIEF SLUG: RUSSIA EUROPE GAS

HEADLINE: Russia Resumes Gas Deliveries Through Pipeline to Europe

Russia imeanza tena usafirishaji wa gesi asilia kupitia bomba la Nord Stream hadi Ulaya leo Alhamisi baada ya kukatizwa kwa shughuli hiyo kwa kipindi cha siku 10, wakati mtambo huo ukifanyiwa ukarabati. Klaus Mueller, mkuu wa wadhibiti wa nishati wa Ujerumani, alituma ujumbe wa Twitter, akieleza kwamba mtiririko wa gesi umefikia 40%, kiwango sawa na kile kilichokuwepo kabla ya ukarabati huo kuanza. Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na serikali ya Russia inadai kwamba kiwango cha gesi kimepungua kwa sasabu mtambo uliokuwa ukifanyiwa ukarabati nchini Canada, haujarejeshwa. Rais wa Russia Vladimir Putin amesisitiza kwamba kampuni ya Gazprom itatimiza majukumu yake, huku akionya kwamba kazi ya kukarabati mtambo huo mwingine, baadaye mwezi huu inaweza kusababisha kupungua kwa kasi ya usafirishaji wa bidhaa hiyo. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametahadharisha juu ya uwezekano wa Russia kukatiza usafirishaji wa bidhaa hiyo, kwa ajili ya kukabiliana na shinikizo la nchi za Magharibi kwa Russia kwa sababu ya uvamizi wake nchini Ukraine.

SRI LANKA POL

Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickre-mesinghe amepishwa Alhamisi kama rais wa taifa lililokumbwa na mzozo, na kuleza mipango yake ya kuunda serikali ya umoja ili kudhibiti machafuko hayo.

Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 73, ambaye alichaguliwa kwa wingi wa kura za wabunge jana Jumatano, kuwa kiongozi wa nchi hiyo, alikula kiapo, huku mkuu wa polisi wa nchi hiyo na mkuu wa jeshi wakisimama nyuma yake.Vyanzo rasmi vya habari vilisema kiongozi huyo mpya anatarajiwa kuunda baraza la mawaziri hivi karibuni litakalojumuisha wabunge kadhaa wa upinzani ili kuiondoa nchi hiyo katika mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi tangu kupata uhuru kutoka kwa Uingereza.

Kiongozi wa upinzani Sajith Premadasa, ambaye alimuunga mkono mgombeaji mpinzani katika kura hiyo ya Jumatano, alisema amekutana na Wickremesinghe kujadili jinsi ya kulinda nchi hiyo dhidi ya "mateso na matatizo" zaidi. "Sisi kama upinzani tutatoa msaada wetu mahsusi, kwa juhudi za kupunguza mateso ya wanadamu," Premadasa aliandika kwneye ukurasa wake wa twitter leo Alhamisi

WORRYING CLIMATE CHANGE PREPAREDNESS

Mataifa yenye uchumi mkubwa kama kama vile India, Brazil na Russia, hayajajitayarisha vilivyo kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na yanakabiliwa na "migogoro" inayosababishwa na hali hiyo, kama vile uhaba wa chakula, nishati na machafuko ya kiraia, ripoti mpya ya utafiti iliyotolewa leo Alhamisi inaonyesha. Will Nichols, mkuu wa hali ya hewa na ustahimilivu katika kampuni ya ushauri ya Verisk Maplecroft, iliyofanya tathmini hiyo, alisema kwamba wakati mataifa yanayoendelea ya Afrika na Kusini-mashariki mwa Asia yanatabiriwa kuathirika zaidi na viwango vya juu vya joto, hali mbaya ya hewa na kupanda kwa kiwango cha bahari, baadhi ya mataifa yenye kipato cha kati yanakosa miundombinu na uhuru wa kutunga sheria ili kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati ulaya inapokadiria gharama ya wimbi lingine la joto lililovunja rekodi, uchambuzi ulionyesha jinsi hata mataifa yaliyo na mizozo michache inayohusiana na hali ya hewa yatahitaji kuzoea, kadiri hali ya joto duniani inavyoongezeka. Utafiti huo uliangalia utendaji wa nchi katika masuala 32 ya kimuundo -- ikiwa ni pamoja na matukio yanayohusiana na hali ya hewa, utulivu wa kisiasa, nguvu za kiuchumi, usalama wa rasilimali, umaskini na haki za binadamu -- kutathmini uwezo wa kila taifa wa kudhibiti migogoro. Chini ya mpango wa utekelezaji wa hali ya hewa unaoongozwa na Umoja wa Mataifa tajiri yaliahidi mwaka 2009 kutoa dola bilioni 100 kila mwaka kwa nchi zilizo hatarini kufikia 2020 lakini hadi sasa yameshindwa hata kufikia kiwango hicho cha ufadhili. Nichols alisema uchambuzi huo unaonyesha haja ya nchi zilizoendelea kusaidia mataifa ambayo hayana uwezo wa kukabiliana na hali hiyo.

NIGER FLOODS

Mafuriko na maporomoko ya ardhi wakati wa msimu wa sasa wa mvua nchini Niger, yamesababisha vifo vya watu 15 na kuathiri wengine zaidi ya 23,000, huduma za ulinzi wa raia zilisema Alhamisi. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Zinder kusini mwa nchi hiyo ya jangwa la Sahel, ikifuatiwa na Maradi na Diffa, ambayo pia ni maeneo ya kusini. Niger, moja ya nchi maskini zaidi duniani kwa kigezo cha umoja wa mataifa cha Maendeleo ya Binadamu, mara nyingi hukumbwa na mafuriko wakati mvua zinazohitajika sana zinapofika.

Msimu huu, ambao unaanza Juni hadi Agosti au Septemba, umekuwa mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na jangwa la kaskazini mwa Niger.

Mwaka jana takriban watu 70 walikufa kote nchini na zaidi ya 200,000 waliathirika kwa njia moja au nyingine, kulingana na takwimu za ndaniya nchi na zile za Umoja wa Mataifa.

UN Kenya elections

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa, wa kutetea haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, leo wametoa wito kwa mamlaka, wagombea na vyama vya kisiasa nchini Kenya kuweka mazingira wezeshi kwa uchaguzi wa amani na kuzuia ghasia zinazohusiana na uchaguzi, wakati nchi hiyo inapojiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 9 Agosti. "Nafasi ya kiraia, ushiriki wa umma, uhuru wa kimsingi na mazingira yasiyo na ghasia ni muhimu ili kukuza ushirikishwaji katika mchakato wa uchaguzi, na utekelezaji wa haki za kisiasa," wataalam walisisitiza. Wataalamu hao, wakiwa ni pamoja na wawakilishi maalum Clement Voule, Mary Lawlor, na Irene Khan, wakitoa taarifa ya pamoja kwa ushirikiano na wengine sita, chini ya programu maalum ya baraza la haki za binadamu, waliwataka washikadau wote nchini Kenya kuheshimu na kudumisha haki ya ushiriki wa kisiasa, uhuru wa kukusanyika, wa maoni na wa kujieleza, na kuheshimu jukumu la mahakama huru katika uchaguzi. Wamesema kuwa mivutano ya kisiasa na ghasia wakati wa kampeni pamoja na matamshi ya chuki na uchochezi wa wagombea na wafuasi wao vina uwezekano wa hatari ya kuhamasisha vurugu. Chaguzi kadhaa za miaka iliyopita zilikumbwa na ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha na unyanyasaji wa kingono na kijinsia. Wasiwasi kuhusu madai hayo ya ukiukaji umeibuliwa na wataalamu kadhaa wa Umoja wa Mataifa katika mawasiliano ya pamoja kwa Serikali ya Kenya kufuatia uchaguzi wa 2017.

XS
SM
MD
LG