Umoja wa Mataifa walaani hatua ya Ethiopia kuwafukuza maafisa wa UN

Your browser doesn’t support HTML5

Jumuiya ya kimataifa yalaani hatua ya Ethiopia kuwafukuza maafisa wa UN

Umoja wa Mataifa Ijumaa umelaani tangazo la Ethiopia la kuwafukuza maafisa saba wa juu wa UN.

Pia umeelezea wasiwasi wake kuhusu watu milioni 5.2 katika mkoa wa Tigray wanaohitaji msaada wa haraka wakati tatizo la utapiamlo linazidi kuongezeka.

“ Nina imani kubwa na wafanyakazi wa UN waliopo Ethiopia wanaofanya kazi hii. UN ina nia ya dhati kuwasaidia watu wa Ethiopia wanaotegemea misaada ya kibinadamu. Sasa tunawasiliana na serikali kuhusu wasiwasi kwamba wafanyakazi wa UN wataruhusiwa kuendelea na kazi yao muhimu,” taarifa ya UN imeeleza.

Marekani na Uingereza ni nchi za mwisho kushutumu uamuzi wa Ethiopia kuwafukuza maafisa saba wa juu wa Umoja wa Mataifa huku ukosoaji wa kimataifa ukiongezeka.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Saki amesema Alhamisi kuwa Marekani haitasita kutumia vikwazo dhidi ya wale wanaovuruga juhudi za kibinadamu nchini humo.

Serikali ya Uingereza imetaka uamuzi huo ubadilishwe haraka.