“Ukurasa mpya mzuri unaandikwa katika historia mpya ya uhusiano kati ya Ukraine na Afrika na Ukraine na Ivory Coast”, naibu waziri wa mambo ya nje Maksym Subkh alisema, kulingana na tasfiri ya hotuba yake ya Kiukreni kwa Kifaransa.
Aliongeza kuwa balozi hizo mpya ni matokeo ya “maagizo ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuimarisha uwepo wa kidiplomasia wa Ukraine barani Afrika.”
Subkh alifungua ubalozi wa Kyiv mjini Kinshasa siku ya Jumatano, huku kukiwa na mipango ya kufungua balozi kadhaa barani Afrika ili kupata uungwaji mkono, wizara ya mambo ya nje ya DRC imeiambia AFP.
Subkh anatarajiwa kufanya ziara nchini Ghana, Msumbiji na Rwanda kuzindua balozi za Ukraine katika wiki zijazo, Mwakilishi wa ubalozi mpya mjini Abidjan ameiambia AFP.