Ujumbe wa Hamas uliwasili mjini Cairo kukutana na mkuu wa idara ya ujasusi ya Misri Abbas Kamel, taarifa ya kundi la Hamas ilisema Jumapili.
Hamas imesisitiza madai iliyotoa katika pendekezo la tarehe 14 Machi kabla ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa la kutaka kusitishwa kwa mapigano katika ukanda wa Gaza ambalo lilipitishwa tarehe 25 Machi.
Madai hayo yanajumuisha sitisho la mapigano la kudumu, kuondoka kwa wanajeshi wa Israel huko Gaza, kurejea kwa waliohama makazi yao, na ubadilishanaji wa wafungwa wa Palestina na mateka wa Israel wanaoshikiliwa Gaza, taarifa hiyo imesema.
Taarifa hiyo imeomba pia msaada kwa Wapalestina na kuanza ujenzi wa Ukanda huo unaokaliwa.