Ukungu uliosababishwa na mashambulizi uliifanya vigumu kuthibitisha hali ilivyokuwa Jumapili, katika vita virefu zaidi tangu uvamizi wa Russia kuanza nchini Ukraine, huku wizara ya ulinzi ya Russia ikiripoti kwamba kikosi cha kibinafsi cha Wagner, kikisaidiwa na wanajeshi wa Russia, kilikuwa kimeuteka mji huo.
Licha ya yote hayo, mji huo mdogo, kwa muda mrefu umekuwa ni wa kuonyesha taswira ya kiishara zaidi kuliko thamani yake ya kimkakati kwa pande zote mbili, kwa mujibu wa wachambuzi.
Kigezo cha kweli zaidi, cha mafanikio kwa vikosi vya Ukraine, kimekuwa uwezo wa wanajeshi wake kuvizuia vikosi vya Russia.
AP inaripoti kwamba jeshi la Ukraine limelenga kumaliza rasilimali na kuwavunja moyo wanajeshi wa Russia katika eneo dogo, lakini muhimu, la kilomita 1,500, huku Ukraine ikijiandaa kwa mashambulio makubwa ya kulipiza kisasi, katika vita hivyo vilivyodumu kwa miezi 15.