Wizara ya nishati ya Uganda imesema kwamba hatua hiyo inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao, ni muhimu wakati nchi hiyo inajitayarisha kuanza kuchimba mafuta ghafi ifikapo mwaka 2025.
Uganda iligundua kuwa na mafuta katika eneo la Albertine, magharibi mwa nchi, miaka 10 iliyopita. Inakadhiriwa kwamba kuna akiba ya mapipa bilioni 6.5 ya mafuta ghafi.
Wizara ya nishati na madini imesema kwamba mazungumzo yanaendelea na makubaliano yanatarajiwa kufikiwa Juni 2023.
Kampuni kadhaa ikiwemo General Electric, ya Marekani, zinatarajiwa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta, chenye uwezo wa kusafisha mapipa 60,000 kwa siku, kwa gharama ya kati ya dola bilioni 3 na 4.
Vitalu vingi vya mafuta nchini Uganda vinamilikiwa na kampuni ya Ufaransa ya Total, CNOOC ya China na kampuni ya mafuta ya kitaifa ya Uganda UNOC.
Uchimbaji wa mafuta katika mradi wa Tilenga, huko Ziwa Albert, utaanza mwezi ujao.