Ripoti hiyo inaeleza kuwa Uganda na msumbiji ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha watu wanaofanya mazoezi. Katika nchi hizi, asilimia 6 pekee ya watu hawafanyi mazoezi
Kutokana na ufinyu wa kipato chao wakiwa wanakwenda kazini, wananchi wa nchi hizo hulazimika kutembea hadi maeneo yao ya kazi kwa kuwa hawana uwezo wa kutumia usafiri wa magari.
Wakati mataifa tajiri, ripoti ya Shirika la Afya Duniania inasema kwamba, watu wengi hufanya kazi zisizo na shughuli nyingi za mwili kama kutumia mashine za dijitali.
Ripoti hiyo imebaini kwamba watu wanaoishi katika nchi tajiri wanafanya mazoezi yenye kuwapa tija kwa kufikia malengo ya afya zao kinyume na wale wanaoishi katika nchi zenye kipato cha chini.
Utafiti mpya unaonyesha kuwa zaidi ya robo moja ya watu wazima kote duniani, sawa na watu bilioni 1.4 hawafanyi mazoezi ya kutosha na hivyo kujieka katika hatari ya kuugua matatizo ya moyo, kisukari na pia baadhi ya saratni miongoni mwa matatizo mengine ya kiafya.
Mwandishi wa Sauti ya Amerika anaelezea kuwa katika ripoti hiyo utafiti wa WHO umewashirikisha karibu watu milioni 2 katika nchi 168 na kugundua kwamba kiwango cha mazoezi kati ya watu wazima hakijabadilika kati yam waka 2001 na 2016.
Shirika la afya duniani linasema kwamba watu hawafanyi mazoezi ya kutosha, jambo linalosababisha wasiwasi hasa kati ya wanawake ambao hawafanyi mazoezi ikilinganiswa na wanaume katika maeneo yote ya dunia kando na maeneo ya mashariki na kusini magharibi mwa Asia.
Kuwait inaongoza kwa idadi ya watu wasiofanya mazoezi kwa asilimia 67, ikifuatiwa na Samoa ya Amerika, Saudi Arabia na Iraq.