Uchaguzi huo umefanyika baada ya wabunge mwezi uliopita kuidhinisha mageuzi yanayounda nafasi mpya ya waziri mkuu ambayo wapinzani wanaamini imewekwa kwa ajili ya kumnufaisha rais Gnassingbe ili kuepuka ukomo wa mihula na kuendelea kukaa madarakani.
Akiwa madarakani kwa karibu miaka 20, Gnassingbe alimrithi baba yake Gnassingbe Eyadema, ambaye aliongoza kwa miongo minne kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika taifa hilo dogo la pwani ya Afrika Magharibi.
Upigaji kura wa leo, utawachagua wabunge 113, na kwa mara ya kwanza manaibu 179 wa mikoa kutoka wilaya tano za nchi ambao pamoja na madiwani wa manispaa watachagua Baraza jipya la Seneti.