Kukabidhiana huko madaraka kupitia uchaguzi ni jambo la historia kwani limetokea mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 59 tangu nchi hiyo ipate uhuru.
“Tunataka kuifanya Congo iwe imara, na kuleta maendeleo kwa njia ya amani na usalama,” amesema kuwaambia maelfu ya wafuasi wake waliokuwa wanashangilia kwenye uwanja wa kasri ya rais. “Congo ya kila mtu, ambapo kila moja ana nafasi ya kushiriki.”
Shamrashamra za tafrija hiyo zilipata mshituko wakati Tshisekedi alipoondolewa jukwaani akiwa hajisikii vizuri alipokuwa akitoa hotuba yake baada ya kuapishwa na hivyo kulazimika kupumzika kidogo.
Lakini alirejea jukwaani muda mfupi baadae akisema kuwa alikuwa amechoka kutokana na kipindi kirefu cha uchaguzi na hisia za tukio hilo muhimu.
Baadaye msemaji wake aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kifaa cha kujilinda na risasi alichokuwa amekivaa kilikuwa kimembana sana.