Trump, Abbas waonyesha dalili za ushirikiano

Rais Donald Trump na Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas

Rais Donald Trump na Kiongozi wa Serikali ya Palestina, Mahmoud Abbas, wameahidi Jumatano wakiwa ikulu ya White House watajaribu kutafuta ufumbuzi wa kidiplomasia katika kufikia amani Mashariki ya Kati.

Wapalestina na Waisraeli lazima washirikiane ilikufikia makubaliano, Trump amesema, akiongeza kuwa, “Nitapenda kuwa msuluhishi au msaidizi, na tutahakikisha hili linafanyika.”

Trump pia ameeleza kuwa katika kipindi cha maisha yake, alikuwa anasikia “kuwa pengine makubaliano magumu kuliko yote kufikia” ni yale kati ya Israeli na Palestina. “Na tuangalie ikiwa tunaweza kuwathibitishia kuwa hawako sahihi, Sawa?”

Akiwa amesimama pembeni yake Rais wa Marekani katika Chumba cha Roosevelt kuzungumza na waandishi, Abbas, akizungumza kwa Kiarabu, amesema anaamini kuwa pande zote zinauwezo chini ya “usimamizi wa kishujaa na uwezo wa kusimamia mazungumzo” wa Trump katika kufikia “makubaliano ya amani ya kihistoria.”

Wakati akimaliza kuongea na kupeana mkono na Trump, Abbas aliongeza kusema kwa Kiingereza: “Sasa, Rais, kwa kushirikiana na wewe, tunamatumaini.”

“Pengine sio zito kiasi hicho”

Dakika chache baadaye wakiwa kwenye Chumba cha Cabinet mlo wa mchana ukiendelea, Trump ambaye alikuwa amefuatana na Makamu wa Rais Mike Pence na Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson, alimwambia Abbas kuwa kufikia makubaliano ya amani “inawezekana ikawa sio jambo gumu kama watu walivyokuwa wanafikiria miaka ya nyuma.”

“Tunaimani kuwa Isreal iko tayari. Tunaimani kuwa wewe pia uko tayari, na kama nyote mko tayari, sisi kwa pamoja tutafikia makubaliano,” Trump aliongeza kusema.

Serikali ya Israeli katika msimamo wake haina uhakika juu ya suluhisho la mataifa mawili wakati ikiendelea na ujenzi wenye utata wa makazi kwa wananchi wake katika maeneo inayo yakalia kwa nguvu na kuendeleza idadi ile ya wakazi wake.

Na kwa upande wa Palestina, Abbas katika nafasi yake kisiasa hana nguvu.

“Hapati ushirikiano mkubwa katika harakati za Palestina, “mchambuzi wa usalama wa taifa Anthony Cordesman wa Kituo cha Mkakati na Tafiti za Kimataifa ameiambia VOA.

Abbas Chama chake chaKisiasa cha Fatah kinakabiliwa na upinzanimkubwa kutoka kwa Hamas, kikundi hasimu cha Palestina kinacho tawala Ukanda wa Gaza