Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:41

Pyongyang yatishika na mazoezi ya 'nyuklia' ya Marekani


Ndege pacha aina ya B-1B Lancer za mashambulizi za Marekani
Ndege pacha aina ya B-1B Lancer za mashambulizi za Marekani

Korea Kaskazini imeituhumu Marekani kwa kuisukuma rasi ya Korea katika ncha ya vita vya nyuklia.

Lalamiko hili limefuatia harakati za ndege pacha za kivita za Marekani na washirika wake Jumanne zilipokuwa zikifanya mazoezi ya kijeshi pamoja na vikosi vya anga vya Korea Kusini na Japan, katika tukio jingine jipya la kuonyesha umwamba.

Ndege mbili za mashambulizi zenye kasi aina ya B-1B Lancer zilipelekwa muda ambapo hali ya utata ukiongezeka kutokana na Korea Kaskazini kukaidi na kuendelea na program yake ya nyuklia na makombora na kupuuzia vikwazo vya Umoja wa Mataifa na shinikizo la Marekani.

Kuruka kwa Ndege hizo mbili Jumatatu kumetokea wakati Rais Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika hali mwafaka, na ni wakati pia Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi akiwasili nchini Korea Kusini kwa mazungumzo.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini Moon Sang-gyun ametoa muhtasari Jijini Seoul Jumatatu kwamba mazoezi ya pamoja yamefanyika ili kuzuia uchokozi unaofanywa na Kaskazini na kufanya majaribio ya uwezekano wa kuwepo vita ya Nyuklia.

Jeshi la anga la Marekani limesema katika taarifa yake ndege hizo za mashambulizi zilikuwa zimeruka kutoka Guam kwa ajili ya kufanya mazoezi na majeshi ya anga ya Korea Kusini na Japan.

Korea Kaskazini imesema ndege za mashambulizi zilifanya “majaribio ya kudondosha mabomu ya aina ya "nyuklia" dhidi ya vituo vikuu” katika eneo lake wakati ambao Trump na wapenda vita wengine wa Marekani wakitaka kuwepo na shambulizi la kuiwahi nchi hiyo isifanye shambulizi la nyuklia” la kushitukiza kutoka upande wa Kaskazini.

“Vitendo vya uchokozi wa kijinga unapelekea rasi ya Korea kuingia karibu kabisa na ncha ya vita vya nyuklia,” Shirika la habari la KCNA la serikali la Kaskazini limesema Jumanne.

Mgogoro katika rasi ya Korea umeongezeka kwa wiki kadhaa sasa, ukisukumwa na wasiwasi kwamba Kaskazini inaweza ikafanya jaribio lake la sita la nyuklia kwa kukaidi shinikizo la Marekani na mshirika pekee wa Pyongyang ambaye ni China.

XS
SM
MD
LG