Makamu Rais Kamala Harris, ambaye pia yuko katika kiyang’anyiro cha White House, alijiunga na wale ambao walikuwa wakishutumu ziara ya Trump na kudai ilikuwa ni ‘kujionyesha kisiasa.’
Sheria ya serikali kuu na sera za Pentagon na hivyo inaweza kusababisha ugomvi na mfanyakazi katika makaburi hayo.
Siku ya Jumamosi, Harrisi alizungumzia suala hilo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, ambao zamani ilijulikana kama Twitter. “Wacha niwe wazi: rais wa zamani haijaiheshimu sehemu takatoifu, yote kwa kutaka sifa ya kisiasa.”
Trump, mgombea urais wa Republican, alirejea kukabiliana na hoja za Jumamosi kwamba alikuwa huko kwa ukaribisho wa jamii wa wanajeshi ambao walifariki katika shambulizi la kigaidi wakati wa Marekani ilipojiondoa Afghanistan mwaka 2021.
“Waliniambia, unajua, sishangazwi, sijawahi hata kufikiria kuhusu hilo. Bwana, je unaweza kupiga picha na sisi kwenye kaburi la mtoto wangu? Nilisema kabisa bila shaka. Sikufanya hivyo kwasababu ya kupata umaarufu. Ninajulikana sana,” alisema Trump.
Kampeni ya Trump ilitoa taarifa na kanda za video siku ya Jumapili kuwa baadhi ya familia za Gold Star ziliunga mkono ziara yake.
Seneta Mrepublican Lindsey Graham alipoulizwa na kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha This Week iwapo kama alidhani kampeni ya Trump ilivuka mpaka.
Alisema, “Mimi naangalia kile ambacho kimetokea. Lakini unafahamu kwa kweli ni bahati mbaya, familia zote hizi zilikwenda kuwatembelea wapendwa wao huko Arlington kutokana na uzembe uliofanywa na utawala wa Biden. Kuongezeka kwa ugaida, ukichanga kwamba mpaka hauna ulinzi, 9/11 nyingine iko njiani inakuja.”
Linapokuwa suala la kulinda mpaka, mtizamo wa Harris huenda ukathibitisha kuwa na mafanikio zaidi, amesema Gavana wa Colorado Jared Polis, aliulizwa kufafanua kama itajumuisha kujenga ukura na utalinganishwa vipi na mwelekeo wa Trump.
Gavana huyo wa chama cha Democrat pia amesema kuwa “Ukuta mpakani ambao Donald Trump alipendekeza ilikuwa ni bahati nasibu kubwa na kupoteza fedha za walipa kodi. Alizungumza sana kuhusu ukuta kwenye mpaka wote badala ya kutumia vizuizi vya aina tofauti vyenya manufaa.”
“Kamala Harris anachosema ni kuulinda mpaka katika gharama ambazo ni nafuu sana kwa njia inayowezekana,”aliongeza
Jumatatu katika sikukuu ya Wafanyakazi, Makamu Rais Harris atafanya kampeni huko Michigan na Pennsylvania. Siku ya Jumanne, kampeni ya itazindua ziara ya basi inayojulikana “Kupigania Uhuru wa Haki za Uzazi”, kwa tukio la kwanza huko Palm Beach, Florida.
Kampeni ya Trump na Vance watakuwa na matukio yao kesho Jumanne huko Braselton, Georgia na Mesa, Arizona.