Uamuzi wa kujiunga na TikTok huenda ukamsaidia Trump kuwafikia wapiga kura vijana, wakati anapojaribu kurejea White House kupitia uchaguzi wa Novemba 5, dhidi ya rais wa sasa Joe Biden.
Tayari timu ya kampeni ya Biden ipo kwenye TikTok, ingawa kiongozi huyo ametia saini mswaada unaolenga kupiga marufuku App hiyo inayotumiwa na takriban wamarekani milioni 170, iwapo mmiliki wake ByteDance kutoka China, hatokubali sehemu yake ya kiutawala iwepo Marekani.
Kampuni hiyo imepinga hatua hiyo mahakamani, ikihitajika kuuza tawi lake la Marekani kufikia Januari mwaka ujao, la sivyo TikTok ipigwe marufuku Marekani. Kampuni hiyo imesema kuwa kamwe haitatoa data za watumiaji wa Marekani kwa serikali ya China, na kwamba tayari imeweka mikakati inayozuia hilo kufanyika.