Trump anatarajiwa kurejea mahakamani Jumatano

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa mahakamani New York wakati kesi ya ulaghai inayohusu biashara zake ilipokuwa ikisikilizwa wiki hii New York.

Mwanasheria mkuu wa New York anatarajia kuthibitisha kwamba Trump alitumia utajiri wake kudanganya kuhusu biashara yake kubwa ya majumba.

Alimshutumu Trump, watoto wake wawili wa kiume wakubwa, na wengine kwa kuongeza thamani kwenye mali zake kwa zaidi ya muongo mmoja, ili kupata mikopo kwenye benki na masharti ya bima, na kuongeza sifa ya utajiri wa Trump kwa zaidi ya dola bilioni 2.

Mapema, shahidi wa kwanza wa serikali Donald Bender, mhasibu wa zamani wa Trump wa Mazars USA alianza tena kutoa ushahidi wake akibaini kwamba taarifa za kifedha alizozitayarisha kwa ajili ya shirika la Trump zilitegemea sana takwimu alizoziripoti mwenyewe.

Wakati huohuo jaji katika kesi hiyo tayari alitoa hukumu kwamba Trump alifanya ubadhirifu na kufuta vyeti vya biashara kwa makampuni yanayodhibiti vito vya thamani vya kampuni za Trump, ikiwemo Trump towers, katika 40 Wall Street katikati mwa jiji la Manhatan.

James anatafuta angalau faini ya dola milioni 250, marufuku ya kudumu dhidi ya Trump na wanawe Donald Jr na Eric kuendesha biashara New York na marufuku ya miaka mitano ya mali isiyohamishika ya kibiashara dhidi yake Trump na shirika lake.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.