Trump anatarajiwa kumtangaza jaji wa kujaza nafasi ya hayati Ginsburg

Amy Coney Barrett

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kumteua Amy Coney Barrett Jumamosi kuchukua nafasi ya jaji wa Mahakama ya Juu ilioachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji mliberali Ruth Bader Ginsburg.

Kifo cha Ginsburg kimempa fursa Trump kuifanya mahakama iwe ya Waconservative zaidi chini ya wiki sita zijazo kabla ya uchaguzi wa rais kufanyika.

Vyombo vya habari mbalimbali vya Marekani, ikiwemo CNN na The New York Times, wametaja vyanzo vya siri Ijumaa vikisema Trump ana azma ya kutangaza jina la Barret kama chaguo lake Jumamosi saa 11 jioni.

Hata hivyo wametahadharisha kuwa mpaka itakapotangazwa kwa umma, kuna uwezekano kuwa Trump anaweza kufanya mabadiliko dakika ya mwisho. VOA haikuweza kuthibitisha ripoti hizi za vyombo vya habari juu chaguo hili.

APTOPIX Trump

Trump ameahidi kumchagua mwanamke kumrithi Ginsburg, aliyekufa wiki iliopita akiwa na umri wa miaka 87.

Iwapo Trump ataamua kumteua mwanamke kuwa mrithi wa Ginsburg, kuna uwezekano mkubwa Barret atapewa kipaumbele, Malcolm amesema.

Barrett, miaka 48, aliteuliwa katika mahakama ya rufaa ya serikali kuu kwa wilaya ya saba mwaka 2017.

Uamuzi wa rais kufanya uteuzi kabla ya kinyang’anyiro cha urais chenye ushindani mkubwa kufanyika ili achaguliwe tena akishindana na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden kimesababisha mvutano wa kisiasa mkali mjini Washington.

Wakati mvutano unaendelea viongozi Warepublikan katika
Baraza la Seneti wakidai mchakato wa kumthibitisha mteule huyo uendelee kwa haraka iwezekanavyo na Wademokrat wanataka uteuzi huo usubiri mpaka mshindi wa uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba atakapojulikana.