Trump anasema Ukraine itashirikishwa katika mazungumzo ya amani na Russia

Rais Donald Trump na Rais Volodymyr Zelenskiy

Rais wa Marekani Donald Trump Alhamisi alisema kwamba Ukraine itashirikishwa katika mazungumzo ya amani na Russia, licha ya kuwa Kyiv imesema ni mapema mno kuzungumza na Moscow kwenye mkutano wa usalama leo Ijumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari White House, Trump alisema Ukraine itakuwa na nafasi mezani katika majadiliano yoyote ya amani na Russia ili kumaliza vita.

“Wanahusika kwenye mazungumzo. Tutakuwa na Ukraine, na tutakuwa na Russia, na tutakuwa na watu wengine watakaoshiriki, watu wengi,” Trump alisema.

Alipoulizwa iwapo anamuamini Putin, Trump alisema “Naamini kwamba atataka kuona kitu fulani kinafanyika. Namuamini kuhusu suala hilo.”

Trump alisema maafisa wa Marekani na Russia watakutana Ijumaa hii huko Munich na kwamba Ukraine ilialikwa pia.