Mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Total Energies, Patrick Pouyanne ambaye pia ni mkurugenzi mkuu amesema Jumatano kwamba anapanga kuzuru Msumbiji baadaye mwezi huu kwa ajili ya mpango wa kuwekeza nchini humo.
“Mradi wetu bado una faida, na tutaendelea nao,” Pouyanne alisema kwenye hotuba yake. Mradi huo wa gesi unakadiriwa kugharimu takriban dola milioni 20, ingawa umecheleweshwa kutokana na ukosefu wa usalama nchini humo.
Pouyanne hata hivyo amesema kuwa hatua kubwa zimepigwa katika kurejesha usalama. Uchaguzi wa rais wa Msumbiji utafayika Oktoba 9 wakati chama cha Frelimo kikitarajia kuendelea na utawala wake uliodumu kwa nusu karne.
Chama hicho kimekuwa kikikabiliana na wanamgambo wa Kiislamu kwenye eneo lenye utajiri mkubwa zaidi wa gesi barani Afrika.