Uchaguzi ulikuwa umepangwa kufanyika Aprili 20, lakini serikali iliuahirisha ikisema majadiliano yalikuwa yanahitajika kuhusu mageuzi hayo, ambayo vyama vya upinzani viliyataja kuwa njama za kutaka Rais Faure Gnassingbe aendelee kukaa madarakani kwa muda mrefu.
“Tarehe ya uchaguzi wa bunge na mikoa ni Jumatatu, Aprili 29,” taarifa ya ofisi ya rais ilisema baada ya mkutano wa baraza la mawaziri jana Jumanne.
Marekebisho hayo ya katiba yalizua mjadala juu ya utawala wa Gnassingbe, ambaye amekuwa madarakani tangu 2005 baada ya kumrithi baba yake aliyetawala kwa miongo mitatu baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Vyama vya upinzani havikutoa taarifa mara moja kuhusu tarehe mpya ya uchaguzi.
Lakini taarifa ya baraza la mawaziri imejiri siku chache kabla ya vyama vya upinzani kupanga kuanda maandamano dhidi ya mageuzi ya katiba na kuahirishwa kwa uchaguzi.