Makundi ambayo hayakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais wa februari 25 yanatia wasiwasi kwa serikali ya mpito wakati rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari akiondoka madarakani rasmi mwezi Mei.
Mohamed alisema “ hakuna msingi” wa katiba ya serikali ya mpito . alisema vyama vya siasa vya upinzani vina haki ya kupinga uchaguzi wa rais mahakamani.
Wagombea wanne wa urais walifungua mashitaka machi 21 kupinga ushindi wa Tinubu kwa madai ya kuenea kwa wizi wa kura na udanganyifu wa kura.
Inachukua takriban miezi minane kwa mahakama kuamua malalamiko ya uchaguzi wa rais. Malalamiko lazima yasikillizwe ndani ya siku 180 tangu siku yalipowasilishwa . mlalamikaji anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa ndani ya siku 21 tangu tarehe ya uamuzi.