Tinubu ashauri viongozi wa Afrika Magharibi kujaribu njia zote za kidiplomasia kurejesha utawala wa kikatiba

Rais wa Nigeria Bola T

Amesema juhudi hizo zifanyike ikiwemo mazungumzo na viongozi wa mapinduzi huko wakati ambapo mkutano wa wakuu wa nchi umeanza Alhamisi.

Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi- ECOWAS lazima iamue jinsi ya kuujibu utawala wa kijeshi ambao walikaidi masharti ya Agosti 6 kuwa ni siku ya mwisho ya kubatilisha mapinduzi na badala yake wakaamua kufunga njia za anga na kuapa kuitetea nchi dhidi ya uvamizi wa kigeni.

Wakuu wa majeshi wa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi walipokutana Abuja, Nigeria, Agosti. 4, 2023, kuijadili Niger.

Wakuu wa ulinzi wa ECOWAS wiki iliyopita waliandaa mipango ya uwezekano wa kuingilia kati kijeshi Niger ambapo wakuu wa nchi watalifikiria katika mkutano wao unaofanyika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, lakini Tinubu alitoa matamshi ya maridhiano zaidi katika hotuba yake ya ufunguzi.

“ Lazima tuzihusishe pande zote zinazohusika , ikiwemo viongozi wa mapinduzi katika majadiliano ya dhati na kuwashawishi kuachia madaraka na kumrejesha rais Mohamed Bazoum ,” Tinubu alisema.

Alielezea mapinduzi ya Julai 26 ya kijeshi nchini Niger , Afrika Magharibi na Kati ni ya saba katika kipindi cha miaka mitatu ikiwa ni tishio kwa uthabiti wa kieneo na kusema lazima njia zote za mawasiliano zitumiwe kuhakikisha kurejea haraka kwa utawala wa kikatiba.