Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:40

Viongozi wa kijeshi Niger wametaja serikali mpya yenye mawaziri 21

Jenerali Abdourahmane Tiani (L) ambaye alijitangaza kiongozi mpya wa kijeshi Niger
Jenerali Abdourahmane Tiani (L) ambaye alijitangaza kiongozi mpya wa kijeshi Niger

Kulingana na amri iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, serikali ya kijeshi iliwataja mawaziri 21. Viongozi watatu wa mapinduzi walitajwa kuongoza  wizara za ulinzi, mambo ya ndani, na michezo.

Viongozi wa kijeshi nchini Niger wameitaja serikali mpya wakati viongozi wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wakikutana katika nchi jirani ya Nigeria kwa kikao cha dharura.

Kulingana na amri iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, serikali ya kijeshi iliwataja mawaziri 21. Viongozi watatu wa mapinduzi walitajwa kuongoza wizara za ulinzi, mambo ya ndani, na michezo.

Hakuna mipango zaidi iliyotolewa katika tangazo hilo. Kutajwa kwa serikali mpya dharau ya karibuni kwa viongozi wa kikanda na inafuatia ukaidi wa utawala kijeshi kupuuza tarehe ya mwisho ya Jumapili ya kumrudisha madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Viongozi wa ECOWAS waliwasili katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, Alhamisi kujadili mzozo wa Niger na kukubaliana juu ya mpango wa kuchukua hatua. Jumuiya hiyo ya kikanda imesema huenda ikatumia nguvu kama ikibidi kurejesha tena demokrasia nchini Niger.

Forum

XS
SM
MD
LG