Tamko hilo limetolewa leo jumamosi na mwanasheria wa THDR, Deogratius Bwire baada ya kukamatwa kwa mratibu huyo katika hoteli ya Blue Pearl saa tatu asubuhi.
Kitendo hicho kimetokea wakati viongozi hao wakiwa wanajiandaa kuingia kwenye uzinduzi wa kitabu cha 'sauti ya watetezi wa haki vyuoni '.
Bwire amesema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kukamatwa kwao baada ya wakili Jones Semdodo aliyoko kituo cha polisi cha magomeni kusema hakuna makosa yaliyoainishwa na wanasubiri maelezo kutoka juu.
Amesema serikali na vyombo vya dola zifanye shughuli zao kihalali pasi na kuonea watu ambao wanafanya shughuli zao kihalali.
Lakini baadhi ya vyanzo vya habari vimesema tayari kiongozi huyo ameachiwa kwa dhamana.