Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:23

Magufuli aagiza Jeshi la Polisi kujipanga upya


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetakiwa kujipanga upya katika safu yake ya makamanda, viongozi wakuu wa vikosi na maofisa mbalimbali.

Mkakati huu ni kuliwezesha kukabiliana na uhalifu na kuondoa dosari zote za utendaji zinazohusiana na ufanisi na heshima ya jeshi hilo.

Aidha, makamanda, maofisa na askari wa jeshi hilo, wametakiwa kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslahi binafsi, kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.

Rais John Magufuli alilitaka pia jeshi la polisi nchini kutumia weledi wake kwa kiwango cha juu katika kutekeleza jukumu lake la kulinda raia na mali zao, hasa kukomesha vitendo vya uhalifu.

Alilipongeza jeshi hilo kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu, lakini alilitaka liongeze juhudi hizo hususani kukabiliana na matukio ya ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija katika mikoa yote.

Wakati akikutana na makamanda wa nchi nzima Rais Magufuli aliwataka maofisa na askari polisi wote wampe ushirikiano wa kutosha IGP Sirro, ambaye hivi karibuni amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, na Meja Jenerali mstaafu Projest Rwegasira

XS
SM
MD
LG