Uingereza imeziwekea vikwazo biashara ambazo imesema zinahusishwa na makundi ya kijeshi yanayopigana katika vita vinavyoendelea nchini Sudan.
Serikali imesema kwamba imeweka vikwazo kwa makampuni sita ya biashara, yanayohusishwa na viongozi katika pande zote zinazohusika na mapigano hayo.
Vikwazo hivyo vimetolewa baada ya ripoti kuonyesha kwamba idadi ya watu ambao wamekoseshwa makao kutokana na mapigano hayo imezidi wtu milioni 3.
Kampuni zilizowekewa vikwazo zinahusishwa na kikosi cha RSF. Miongoni mwao ni Al-Junid, ambayo serikali ya Uingereza imesema kwamba ilitoa mamilioni ya pesa kwa makundi ya wapiganaji, kampuni ya GSK na Tradive General.