Kwa upande wa pili Kiir alitia saini rasimu kama hiyo jana Jumanne huko Khartoum lakini Machar alikataa kutokana na kua na mashaka juu ya idadi ya majimbo na mipaka yao.
Machar alitia saini rasimu ya awali ya mkataba wa kushirikiana madaraka mwanzoni mwa mwezi Agosti katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum akiwa na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.
Utawala wa Kiir ulibadilisha idadi ya majimbo yaliyokuwepo hapo 2015 kutoka 10 hadi 32.
Lakini saa kadhaa baadae, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Al-Dierdiry Ahmed aliwaambia waandishi wa habari kwamba Machar alibadilisha mawazo yake na atatia saini mkataba kesho Alhamisi baada ya majadiliano ya kina na wapatanishi wa Sudan.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Mkamiti Kibayasi, Washington, DC