Shirika hilo lenye makao yake New York lilianza orodha hiyo miaka 15 iliyopita kama zana ya mipango ya ndani ya kujiandaa kwa mwaka ujao, lakini mkurugenzi mtendaji David Miliband amesema kwa sasa orodha hiyo pia inatumika kama wito wa kuchukua hatua duniani kote.
Ripoti hiyo imesema watu milioni 305.1 duniani kote wanahitaji misaada ya kibinadamu, ni wengi zaidi ikilinganishwa na watu milioni 77.9 mwaka 2015, na kwamba asilimia 82 ya watu hao ni kutoka nchi 20 ambazo ziko kwenye orodha ya IRC.
Miliband ameelezea idadi hiyo kuwa inatisha.
Ripoti hiyo imesema mzozo wa kibinadamu nchini Sudan ndio mbaya zaidi na asilimia 10 ya watu wote wanaohitaji msaada ni kutoka nchi hiyo, licha ya kuwa ni makazi kwa asilimia 1 tu ya idadi ya watu duniani.