Tishio la kuongezeka tena kwa mashambulizi lilikuja wakati mwanadiplomasia mkuu wa Washington, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, alipokutana na maafisa wa Israeli kutafuta sitisho la muda mrefu katika mzozo huo mbaya. Kwa mara nyingine tena hatma ya sitisho la mapigano haijulikani.
Chanzo cha Hamas kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa mateka wengine 10 wa Israel wataachiliwa kutoka Gaza kwa mabadilishano ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel, baada ya pande zinazozozana kukubaliana kuongeza muda wa sitisho la mapigano hadi Ijumaa asubuhi.
Wakati huo huo Wapatanishi Misri na Qatar wanashinikiza kuongezwa kwa siku mbili zaidi kwa makubaliano ya sitisho la muda la mapigano huko Gaza pamoja na kuachiliwa zaidi kwa wafungwa pamoja na ongezeko la upelekaji wa misaada ya kibinadamu, taarifa kutoka chombo cha habari cha serikali ya Misri kimesema Alhamisi.
Juhudi hizo zinafuatia ongezeko la dakika ya mwisho siku ya Alhamisi za sitisho kwa siku ya saba
Ongezeko la Alhamisi ni pamoja na kuachiliwa kwa Waisraeli 10 waliotekwa na Hamas na wafungwa 30 wa Kipalestina, pamoja na utoaji wa viwango sawa vya misaada ya kibinadamu kama ilivyokuwa siku sita zilizopita, mkuu wa idara ya habari ya serikali ya Misri Diaa Rashwan, alisema katika taarifa.
"Misri itaendelea kufanya juhudi zake zote kuhakikisha
mtiririko wa misaada ya kibinadamu inaendelea kuelekea kaskazini na kusini mwa Ukanda wa Gaza," ilisema taarifa hiyo.