Mahakama ya juu nchini Ghana Jumatano imetupilia mbali rufaa mbili za kubatilisha kifungu cha sheria kilichokuwa kimepingwa kwamba kinakandamiza vikali haki za wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo ilipitishwa na wabunge mapema mwaka huu.
Wabunge walipitisha mswada huo, the Sexual Rights and Family Values mwezi Februari, uliokosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa licha ya kuungwa mkono na watu wengi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Sheria hiyo inapendekeza kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa watu wa jinsia moja wanaotenda ngono na hadi miaka mitano jela kwa kutangaza au kufadhili shughuli za watu wa jinsia moja.
Mswada huo utakuwa sheria baada ya kusainiwa na rais Nana Akufo-Addo ambaye bado hajatangaza uamuzi wake.