Sherehe za kumuenzi Seneta McCain ndani ya jengo la Bunge la Marekani

Jeneza la Seneta John McCain likiwa katika jengo la Bunge la Marekani, Agosti 31, 2018, mjini Washington.

Mvua ikinyesha wakati makundi ya watu wakingojea kuingia katika jengo la Bunge kutoa heshima zao za mwisho kwa Seneta John McCain aliyefariki Agosti 25.

Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnel wa Kentucky akiongea wakati wa sherehe za kumuenzi Seneta John McCain akiwa ndani ya jengo la Bunge la Marekani Agosti 31, 2018, mjini Washington.

Kumbukumbu: John McCain wakati alipojeruhiwa akitumikia Jeshi la majini la Marekani huko Vietnam Kaskazini.

Cindy McCain, wife of the late U.S. Senator John McCain, stands over his casket as he lies in state in the U.S. Capitol Rotunda, Washington
Mjane wa Seneta John McCain, Cindy McCain, akiwa amesimama mbele ya jeneza la mumewe ndani ya jengo la Bunge la Marekani, Washington.

Seneta wa Marekani Lindsey Graham akitoa heshima zake za mwisho wakati wa sherehe za kumuenzi Seneta aliyeaga dunia John McCain ndani ya jengo la Bunge la Marekani, mjini Washington.

Roberta McCain, mwenye umri wa miaka 106, mama mzazi wa Seneta John McCain wa Arizona, akiwa mbele ya jeneza lililo funikwa kwa bendera ya Marekani ndani ya jengo la Bunge la Marekani wakati wa sherehe za kuuaga mwili wa marehemu, Ijumaa, Agosti. 31, 2018, mjini Washington. 

Spika wa Bunge la Marekani Paul Ryan (kati) amesimama pamoja na Kiongozi wa walio wengi katika Seneti, Mitch McConnel (kushoto) na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence (kulia) katika ukumbi wa Rotunda wa Bunge la Marekani muda mchache kabla ya kuanza hafla ya kumuenzi Seneta John McCain ambaye ameaga dunia.

Mwili wa Seneta John McCain ukienziwa ndani ya Jengo la Bunge la Marekani.