Sherehe za kuapishwa Rais Joe Biden na Makamu Rais Kamala Harris

Joe Biden akiapa kuwa  rais wa  46th wa Marekani mbele ya Jaji Mkuu John Roberts huku mkewe Jill Biden akishikilia Bibilia nje ya Jengo la Bunge la Marekani. 

Rais Joe Biden akihutubia baada ya Kula kiapo nje ya Congress, Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021.(AP Photo/Patrick Semansky, Pool)

Rais mteule Joe Biden, mkewe Jill Biden na Makamu Rais mteule Kamala Harris na muwewe Doug Emhoff wakiwasili Bungeni kwa ajili ya sherehe rasmi za kuapishwa mjini Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021. (AP Photo/J. Scott Applewhite)

Kamala Harris akiapishwa kuwa Makamu Rais na Jaji wa Mahakama ya Juu Sonia Sotomayor huku mumewe Doug Emhoff akishikilia Bibilia Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021. (AP Photo/Patrick Semansky, Pool)

Rais mteule Joe Biden na Makamu Rais Kamala Harris wakati wakijiandaa kuapishwa nje ya Bunge la Marekani, Washington, U.S., January 20, 2021. REUTERS/Brendan McDermid

Rais Joe Biden akila kiapo kuwa Rais wa 46 Marekani, Januari 20, 2021. Saul Loeb/Pool via REUTERS

Kamala Harris akila kiapo kuwa Makamu Rais wa Marekani, nje ya Bunge la Marekani, Washington, U.S., January 20, 2021. REUTERS/Kevin Lamarque

Makamu wa Rais Kamala Harris akifurahia kuapishwa kwa Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa Marekani. REUTERS/Brendan McDermid

Rais wa zamani Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakiwasili katika sherehe za kuapishwa  Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa Marekani.

Msanii Lady Gaga akiwasili kuimba mwimbo wa taifa katika sherehe za kuapishwa Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa Marekani.20, 2021. REUTERS/Jim Bourg

Rais wa Marekani Joe Biden, mkewe Jill Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris, na mumewe Doug Emhoff mara baada ya zoezi la kuapishwa kumalizika, Washington, Marekani., Januari 20, 2021. REUTERS/Tom Brenner

Joe Biden ameapishwa Jumatano kuwa Rais wa 46 wa Marekani pamoja na Makamu Rais Kamala Harris, Seneta wa zamani Baraza la Seneti la Marekani.