Shambulizi la kombora katika soko la Sennar kusini mashariki mwa Sudan liliua watu 21 na kujeruhi wengine 67 Jumapili, chanzo cha matibabu kimeiambia AFP, kikilaumu wanamgambo kuhusika na shambulizi hilo.
Chama cha madaktari wa Sudan, ambacho kilianzishwa baada ya vita kuanza mwezi Aprili mwaka 2023 kimeripoti idadi hiyo hiyo ya vifo, lakini kimesema idadi ya waliojeruhiwa ni zaidi ya 70. Kimekilaumu kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) kwa kufanya shambulizi hilo la kombora.
RSF inayoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo, inapambana na jeshi la Sudan chini ya uongozi wa Abdel Fattah al-Burhan.
Serikali hapo awali ilishtumu RSF kwa kulenga raia na taasisi za kiraia.