Sweden yaomboleza shambulizi la kigaidi lilouwa watu wanne

Maua na mishumaa imewekwa katika mtaa ambao shambulizi lililofanyika huko Sweden

Taifa la Sweden lilifanya maombelezo kwa kukaa kimya dakika moja Jumatatu kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la kigaidi lililotokea Ijumaa ambapo watu wanne waliuawa na wengine 15 kujeruhi.

Raia wa Uzbek mwenye umri wa miaka 39 ambaye inasadikiwa alikuwa anasikitiko kwa wale wenye siasa kali amewekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kuendesha gari kwa nguvu, alilokuwa ameiba, kwenye kundi la watu katika duka kubwa la Ahlens huko Stockholm.

Jumapili, maelfu ya watu wa Sweden walijitokeza siku ya Jumapili Stockholm kwa kile walichokiita “kuimarisha upendo” kati yao baada ya shambulizi hilo.

“Hatuwezi kuruhusu uoga ututawale. Ugaidi hauwezi kushinda, “Meya Karin Wanngard ameliambia kundi la watu takriban 50,000.

Mwanamke mmoja alikuwa ameshikilia bango lililosoma: “Hatuwezi kujibu mashambulizi haya kwa uonga, tunajibu kwa upendo.”

Polisi wamemkamata mzaliwa wa Uzbek ambaye ni mshukiwa katika tukio hilo, masaa kadhaa baada ya shambulizi hilo.

Alikuwa anajulikana na vyombo vya upelelezi tangia mwaka jana baada ya kutoweka kabla ya hatua za kumuondoa nchini kukamilika, mara ombi lake la kubakia kama mkimbizi lilipokataliwa.

Vyombo vya dola vilikuwa vinafahamu kwamba alikuwa na sikitiko juu ya watu wenye siasa kali.

Hata hivyo hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo la Ijumaa na wala sababu ya ushawishi wa kutenda hilo.

Polisi wanasema wamemkamata mtu wa pili kuhusiana na shambulizi hilo, lakini hawakutoa maelezo zaidi.

Picha zilizochukuliwa katika eneo la tukio Ijumaa zilionyesha gari hilo ni lori ambalo linamilikiwa na kampuni ya kutengeneza bia Spendrups, kampuni hiyo ilisema lori lake lilikuwa limetekwa mapema siku hiyo ya tukio.

Walioshuhudia tukio wanasema kuwa lori hilo liliingia moja kwa moja katika lango kuu la duka kubwa la Ahlens upande wa Drottninggatan, mtaa mkubwa unaotumiwa na watembea kwa miguu.

Imeripotiwa watu waliokuwa wakifanya manunuzi walipiga makelele na kukimbia. Picha za Television zilionyesha moshi ukitoka katika duka hilo baada ya ajali hiyo.