Shambulizi la kigaidi London laua 7, askari waua washukiwa 3

Magari ya polisi yazingira daraja la London baada ya shambulizi

Askari Jijini London wamesema mapema Jumapili kuwa watu saba na wengine watatu waliowashambulia wamepoteza maisha katika tukio la hivi karibuni la kigaidi huko Uingereza.

Gari kubwa la kusambaza bidhaa liliwagonga kwa makusudi watu waliokuwa wanatembea kwa miguu katika mwendo kasi kabisa kwenye Daraja la London jioni Jumamosi, na kuelekea kwenye soko la Borough ambako watu watatu walilitelekeza lori hilo na kuwachoma visu watu kadhaa.

Polisi wamesema kuwa watu hao watatu walioshambulia waliuawa na maafisa wa polisi katika dakika nane mara tu habari zilipofika kwenye chumba cha dharura. Polisi wamesem kuwa mabomu yaliyokuwa yamevaliwa na washambuliaji hao, yakiwafanya waonekane kama ni wanaojitoa muhanga, yalikuwa ni feki.

Gari kubwa la kusambaza mizigo lililokuwa katika mwendo kasi liliwagonga watembea kwa miguu katika daraja la London jioni Jumamosi katika kile kilichoelezwa ni shambulizi la kigaidi.

Katika tukio hilo watu kadhaa walijeruhiwa na walikuwa pembeni ya barabara wakitokwa na damu katika mji mkuu wa Uingereza.

Karibu na eneo la tukio hilo la kigaidi barabarani, washambuliaji pia waliwachoma watu kwa visu.

Huduma ya magari ya wagonjwa London imesema kupitia Twitter kuwa iliwapeleka sio chini ya watu 20 walioumizwa katika hospital sita mbalimbali London.

Vyombo vya dola vimetangaza kuwa tukio hilo ni la kigaidi. Maaskari wenye silaha nzito walifanya upekuzi katika eneo na kuagiza wanaosimamia mabaa na migahawa kwenda sehemu zenye usalama.

Askari walipiga risasi kadha; walioshuhudia wamesema kuwa washambuliaji wawili walipigwa risasi lakini wengine watatu walifanikiwa kutoroka.

Askari wa Uingereza hapo awali walishuku kuwa ushambuliaji wa kutumia visu uliofanyika London Kusini unaweza kuwa na mafungamano na mashambulizi yaliyokuwa yametokea karibu na Daraja la London.