Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:01

Magaidi watumia lori, visu kuwashambulia watu London


Wanawake wazungumza na waandishi baada ya tukio la kigaidi London.
Wanawake wazungumza na waandishi baada ya tukio la kigaidi London.

Gari kubwa la kusambaza mizigo lililokuwa katika mwendo kasi liliwagonga watembea kwa miguu katika daraja la London jioni Jumamosi katika kile kilichoelezwa ni shambulizi la kigaidi.

Katika tukio hilo watu kadhaa walijeruhiwa na walikuwa pembeni ya barabara wakitokwa na damu katika mji mkuu wa Uingereza.

Karibu na eneo la tukio hilo la kigaidi barabarani, washambuliaji pia waliwachoma watu kwa visu.

Repoti mbalimbali zimesema kuwa zaidi ya mtu mmoja amepoteza maisha, na idadi ya watu waliokuwa wameathirika inategemewa kuongezeka.

Huduma ya magari ya wagonjwa London imesema kupitia Twitter kuwa iliwapeleka sio chini ya watu 20 walioumizwa katika hospital sita mbalimbali London.

Vyombo vya dola vimetangaza kuwa tukio hilo ni la kigaidi. Maaskari wenye silaha nzito walifanya upekuzi katika eneo na kuagiza wanaosimamia mabaa na migahawa kwenda sehemu zenye usalama.

Askari walipiga risasi kadha; walioshuhudia wamesema kuwa washambuliaji wawili walipigwa risasi lakini wengine watatu walifanikiwa kutoroka.

Askari wa Uingereza hapo awali walishuku kuwa ushambuliaji wa kutumia visu uliofanyika London Kusini unaweza kuwa na mafungamano na mashambulizi yaliyokuwa yametokea karibu na Daraja la London.

Lakini tamko la baadae, hata hivyo, lilithibitisha kuwa uchomaji visu huo katika eneo jirani la Vauxhall lilikuwa halina mahusiano.

Shambulizi hilo la kigaidi, ambapo baadhi ya washambuliaji hao walikuwa wametumia visu vilivyokuwa na urefu wa centimeter 25, inawezekana walikuwa wanapanga kutumia mabomu pia.

Picha iliokuwa imepigwa ndani ya eneo lililokuwa limezingirwa na polisi lilimuonyesha mshambuliaji moja akiwa ardhini hawezi kusimama, na idadi ya mikebe yenye vipande vya vyuma viliyokuwa vimefungwa mwilini mwake; wakati, polisi katika eneo hilo walipo yadhibiti baadhi ya mabomu hayo kwa uangalifu.

Mayor wa Uingereza, Sadiq Khan, amelaani shambulizi hilo na kusema yeye na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May watashiriki katika mkutano wa dharura wa kikundi ya kushughulikia migogoro cha Cobra.

“Mpaka sasa hatuna maelezo kamili,” amesema mayor, “Lakini hii ilikuwa ni shambulizi la kukusudia na la kiuoga kwa raia wa London na wale wanaotembelea nchi hii wasiokuwa na hatia.

“Nina laani kwa nguvu zangu zote jambo hili. Hakuna uhalali wowote kwa vitendo hivi vya kinyama.”

Mauaji ya usiku wa Jumamosi katika daraja la London na katika soko la karibu la Borough jirani na hapo ni tukio la tatu la kigaidi Uingereza tangu mwezi Machi.

Kabla ya tukio hili kulikuwa na shambulizi kama hili kwa watembea kwa miguu katika Daraja la Westminster na chini ya wiki mbili zilizopita kulikuwa na shambulizi la bomu huko Manchester.

XS
SM
MD
LG