Shambulizi la jeshi la Israel lililolenga wanamgambo wa Hamas limesababisha kufungwa kwa hospitali kuu huko kaskazini mwa Gaza na kushikiliwa kwa mkurugenzi wake, shirika la afya duniani na maafisa wa afya wamesema Jumamosi.
Shambulizi kwenye hospitali ya Kamal Adwan limesitisha kabisa shughuli katika hospitali hiyo na kufanya hali ya afya huko Gaza kuwa mbaya zaidi, maafisa wa afya katika eneo hilo wamesema.
WHO imesema wahudumu wa afya 60 na wagonjwa 25 waliokuwa katika hali mbaya wameripotiwa kubaki katika hospitali hiyo.
Wagonjwa ambao hawakuwa katika hali mbaya wamelazimika kuondoka kwenye hospitali iliyoharibika na isiyofanya kazi inayomilikiwa na Waindonesia, WHO imesema, ikiongeza kuwa ina wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa wagonjwa hao.