Kijana mwenye umri wa miaka 18, Muhammad Medhat Amin Amer, “ aliuawa kwa risasi za Israel katika kambi ya Balata” katika eneo la kaskazini, wizara ya afya ya Palestina ilisema katika taarifa Ijumaa usiku, ikiongeza kuwa watu tisa walijeruhiwa, “wanne kati yao ni mahututi.”
Kulingana na shirika la Palestina la Mwezi Mwekundu, shambulio hilo lilianza Ijumaa usiku na kusababisha mapambano makali.
Katika taarifa Jumamosi, jeshi la Israel limesema wakati wa “operesheni ya kukabiliana na ugaidi”, “magaidi waliweka vilipuzi katika eneo hilo ili kuwadhuru wanajeshi, kurusha vilipuzi, mabomu ya kienyeji, mawe na kufyatua fataki kwa wanajeshi.