Shambulio la Jumatatu kwenye msikiti limefanyika wakati Washia wanaadhimisha wiki hii Ashura, siku ya maombolezo ya kila mwaka ya kukumbuka kifo cha Imam Hussein katika vita vyake vya karne ya saba, anayechukuliwa na dhebehu hilo kama mrithi wa Mtume Muhammad.
“Polisi wa Ufalme wa Oman wamekabiliana dhidi ya tukio la ufyatuaji wa risasi lililotokea karibu na msikiti katika eneo la Al-Wadi Al-Kabir katika mji mkuu, taarifa ya polisi ilisema.
Washambuliaji watatu waliohusika katika shambulio hilo waliuawa na maafisa wa polisi “walitekeleza utaratibu wa kukabiliana na ufyatuaji wa risasi,” taarifa hiyo iliongeza.
Jeshi la polisi limesema watu 6 waliuawa, akiwemo afisa wa polisi. Limesema watu 28 wenye uraia mbalimbali walijeruhiwa, wakiwemo waokoaji na wanatoa huduma za matibabu.
Kundi la Islamic State limedai kufanya shambulio hilo, likisema wapiganaji wake watatu ndio walifanya ufyatuaji huo wa risasi ambao ulilenga “Washia waliokuwa wanatekeleza ibada yao ya kila mwaka” wakati wa kipindi kitakatifu cha maombolezo Cha Ashura.